EAST AFRICAN COMMUNITY
LAKE VICTORIA BASIN COMMISSION
TANGAZO LA MNADA WA HADHARA
Kampuni ya udalali ya YONO AUCTION MART & CO. LTD kwa idhini ya EAC LAKE VICTORIA BASIN COMMISSION (LVBC) watauza Vifaa vya Meli vilivyotumika siku ya Jumanne tarehe 27/06/2023 Kuanzia saa 4.30 asubuhi. Mnada utafanyika Bandari (Mwanza South).
Vifaa vifuatavyo vilivyotumika vitauzwa:-
Mali zote zinaweza kukaguliwa bandarini (Mwanza South) tarehe 23/06/2023 na 26/06/2023 asubuhi mpaka saa 8.30 mchana.
Masharti ya mnada: mnunuzi wa injini, vipuri, vifaa vya elektroniki, magodoro na mbao anatakiwa kulipa malipo yote au deposit ya 50% pale pale na salio lilipwe ndani ya siku tano (5) kwa Benki. Mwisho wa kulipa ni tarehe 05/07/2023 saa 10:00 jioni. Kama mteja atashindwa kulipa ndani ya siku hizo tajwa hapo juu mali itauzwa kwa mshindi mwingine aliyefata na 50% haitarudishwa.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
East African Community, Lake Victoria Basin Commission New Nyanza Regional Headquarters, 13th floor, Owuor Otiende Road P. O. Box 1510 – 40100, Kisumu, KENYA. Telephone Number: +254 57 2023873 | Mkurugenzi Mtendaji Yono Auction Mart & Co. Ltd NSSF Benjamini Mkapa, Parking Tower S.L.P 10674 Dar Es Salaam, TANZANIA Mwanza Branch Manager: +255 755 092734 |